0

Huko nyuma Rose Muhando alishawahi kuzua utata kwa kutojulikana, ni nani haswa anahaki ya kusambaza kazi zake huko nchini Kenya, jambo lilozua utata mkubwa kutokana na jinsi kazi za mwanamuziki huyu wa nyimbo za dini zilizokuwa na soko hivi Afrika mashariki.Sources zinasema kuwa wasambazaji wa kampuni ya Umoja Audiovisual ilishawasiliana na kampuni ya mwanamuziki aitwaye Japheth Kassanga juu ya usambazaji wa kazi za Rose Muhando nchini Kenya.

Cha kushangaza zaidi mbali na kumwaga wino na kukubaliana kusambaza kazi hizo, kampuni nyingine tena nchini humo ilimfwata Rose muhando kisiri na kusign naye mkataba wa kusambaza kazi zake, na kusababiisha mtafaruku mkubwa kati ya makampuni hayo, hata hivyo inasemekana kampuni zote mbili zinatarajia kukaa chini kusuluhisha utata huo.

Post a Comment

 
Top