Tetesi za chanzo cha mdogo wake Beyonce, Solange kumpiga Jay Z walipokuwa ndani ya lift zinazidi kuzua ripoti kutoka kwa vyanzo mbalimbali.
Kwa mujibu wa The New York Daily News, Solange anadaiwa kuwa
alichukizwa na uamuzi wa Jay Z kutaka kuondoka kwenye After Party
waliyokuwepo na Beyonce na Solange Standard Hotel na kutaka kwenda
kwenye after party ya Rihanna bila Beyonce.
Chanzo kimeiambia Daily News kuwa Solange alimuuliza Jay Z, “kwa nini
huendi nyumbani?” na akamuuliza Beyonce pia, “Kwa nini mumeo anataka
kwenda club muda huu?” Na Jay Z akajibu “You’re one to talk.”
Inaelezwa kuwa jibu la Jay Z lilichochea kwa kiasi kikubwa hasira za
Solange ambaye baadae alizua timbwili la aina yake kwenye lift.
Bado haijathibitishwa chanzo cha Solange kuanza kurusha makofi na
mateke kwa Jay Z kwa kuwa katika video iliyosambaa hakuna sauti yoyote
inayosikika.
Vyanzo vingine vilieleza kuwa Solange alikuwa amelewa sana wakati
wakiwa kwenye after party hiyo na kwamba alizua ugomvi mapema na mgeni
mmoja.
Katika hatua nyingine, imeripotiwa kuwa Jay Z na Solange wameonekana
wakifanya shopping kwenye duka moja la pete Jumanne, May 13.
Inawezekana wameshamaliza tofauti zao kwa kuwa ugomvi wao ulitokea wiki moja iliyopita licha ya video kusambaa wiki hii
Post a Comment