WAKATI viongozi wa kile kinachoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wanaonesha kushikamana hadharani, habari za ndani ya Umoja huo zinasema kuwa mivutano imeanza kuzuka huku baadhi ya viongozi wake wakitaka kurejea Bunge Maalum la Katiba.
Habari
kutoka ndani ya Umoja huo zinasema kuwa angalau viongozi wawili wa
vyama vinavyounda UKAWA wanataka kurejea bungeni na kushiriki mchakato
wa kutunga Katiba mpya wakati Bunge hilo litakapoanza tena Agosti mwaka
huu.
Habari
zinasema kuwa viongozi hao wawili, wanataka kurejea tena bungeni kwa
sababu wameanza kubaini kuwa kuna ujanja mwingi ndani ya UKAWA na kuwa
baadhi ya vyama vinavidanganya na kuvitumia vingine, bila kuonekana kwa
faida yoyote dhahiri.
“Tulisusa
Bunge kwa pamoja, lakini sasa inaanza kuonekana kuwa wapo wenzetu ambao
wana maslahi binafsi na kuonekana kututumia sisi kwa manufaa yao ya
kisiasa na hata kifedha,” anasema mmoja wa viongozi wa UKAWA, ambaye
anahisi baadhi ya wenzao wanapata maslahi zaidi kuliko wengine.
Kuna
madai kuwa UKAWA wamepatiwa fedha, tena nyingi na mfadhili ama
wafadhili wa nje ya Tanzania, lakini fedha hizo zinaishia mifukoni mwa
kiongozi mmoja ama wawili wa umoja huo, usiosajiliwa na unaoendesha
shughuli zake za kisiasa, bila hati zozote za kuuhalalisha kuendesha
shughuli za kisiasa.
Viongozi
wa vyama CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi na vyama vingine vidogo vidogo
walisusa Bunge Maalumu la Katiba mwezi uliopita, wakiazimia kuendesha
kampeni ya kutafuta Katiba mpya nje ya Bunge, kupitia mikutano ya
hadhara ya wananchi. UKAWA walifanya mkutano wao wa kwanza mjini
Zanzibar juzi.
Pamoja
na kwamba ni dhahiri kuwa Umoja huo na shughuli zake haziungwi mkono na
wananchi wa Tanzania walio wengi, lakini viongozi wake wameendelea
kushikilia kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima.
Wachunguzi
wa masuala ya kisiasa, wanasema kuwa UKAWA wamechagua kuanzia mikutano
yao Zanzibar, kwa sababu huko ndiko wana uhakika wa kupata watu wa
kuhudhuria mikutano yao, kwa sababu ya wanachama wa CUF.
“Wamekimbia
Zanzibar kwa sababu huko Bara watampata nani wa kwenda kupoteza muda
wake kusikiliza hoja zisizokuwa na mashiko,” amesema mchunguzi mmoja wa
Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro.
>>Habari leo
>>Habari leo
Post a Comment