IMEELEZWA kwamba, nyota wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ (pichani) anatakiwa kuendelea kuhudhuria kliniki kila siku katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar kwa siku 730 (miaka miwili) bila kukosa hata siku moja kufuatia athari ya matumizi ya madawa ya kulevya kinyume cha hapo ni kuhatarisha maisha yake.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya madaktari ambao
hawakutaka majina yao yatajwe kwa madai kwamba msemaji wa hospitali hiyo
ni mganga mkuu zinaeleza kwamba, mwanamuziki huyo anaendelea vizuri
kiafya tofauti na tetesi za mitaani kwamba amerudia kubwia unga.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Sophinias Ngonyani ambaye alikiri Ray C kuhudhuria kliniki ya hospitali yake na kutakiwa kumaliza muda aliopangiwa wa miaka miwili na endapo atakatisha atadhurika.
“Hapa hospitali mbali na Ray C, kuna waathirika wengine nao wamekuwa wakihudhuria kliniki na wanaendelea vizuri.
“Hata hivyo, Ray C amebakiza miezi michache, tumemwambia asithubutu kukosa kufika kliniki hata siku moja hadi amalize siku zake 730,” alisema mganga mkuu huyo.

Post a Comment