Waethiopia 55 wamekamatwa na wanakijiji cha Chekereni Pabliki kilichopo Himo, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wakiwa wamejificha kichakani na mkazi mmoja wa kijiji hicho.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz,
amethibitisha kutokea tukio hilo na kwamba watu hao walikamatwa ...
“Wanakijiji walitoa taarifa polisi baada ya kuwaona watu hao, na sisi tulifika mara moja kuwakamata wakiwa na mwenyeji wao,” alisema Kamanda Boaz.
“Wanakijiji walitoa taarifa polisi baada ya kuwaona watu hao, na sisi tulifika mara moja kuwakamata wakiwa na mwenyeji wao,” alisema Kamanda Boaz.
Aliongeza: “Kwa sasa hatuwezi kumtaja jina wenyeji wa watu hao kwa vile bado tunaendelea na uchunguzi zaidi.”
Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, watu hao baada ya
kuhojiwa walidai kuwa walikuwa njiani kwenda nchini Afrika Kusini
kupitia Tanzania.
Alisema uchunguzi unaendelea ili kubaini wahusika
wengine zaidi wa mtandao wa kusafirisha binadamu kabla ya kufikishwa
mahakamani.
Aliwataka wananchi waishio mipakani kuendelea kuwa
walinzi na kutoa taarifa polisi pindi wanapowaona watu wanaowatilia
shaka katika maeneo yao.
Post a Comment