0
STAA wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amesema kifo cha msanii mwenzake Rachel Haule ‘Recho’ hakitafutika kichwani mwake kirahisi, kwa kuwa anamkumbuka kwa mengi.
Staa wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ akilia kwa uchungu katika mazishi ya msanii mwenzake katika tasnia ya filamu, Recho Haule.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Sinza – Palestina kulipokuwa na msiba wa Recho, Johari alisema Recho alikuwa na kiu ya kufika mbali na hakuchoka kuomba ushauri na kuufanyia kazi.
Recho haule (kushoto) akiwa na mke wa Mtitu enzi za uhai wake.
“Amefanya kazi na RJ Company muda mrefu, baadaye akaamua kuanza kufanya kazi zake akishirikiana na Saguda. Mwanzo ulikuwa mzuri sana, alikuwa akitaka kitu chake anaweza kupiga simu hadi usiku kuomba ushauri. Kwa kweli sitamsahau, nitamlilia milele,” alisema Johari.

Post a Comment

 
Top