
Kulikuwa na rumors hapo mwanzo kuwa Diamond yupo studio akipika moja
ya colabo matata sana huko nchini sauzi pamoja na kundi la mafikizolo,
na hata baadhi ya picha ali-post akiwa anaonekana yuko studio na kundi
hilo la muziki, umbea huo umesibitishwa tena kuwa na ukweli wa asilimia
mia moja na mmoja wa Dj maarufu hapo south, ambaye ndiye anayesemekana
anasimamia swala zima la nyimbo hiyo, jamaa maarufu sana, anajulikana
kama Oskido, kupitia account yake ya instagram alifunguka kuwa yupo
studio akitengeneza ngoma hiyo.

Oskido ambaye ni mzimbabwe anayefanyia kazi zake za u-DJ afrika ya
kusini, alishawahi anatajwa kuwa ndiye nguli wa kutengeneza kwaito huko
bondeni, aliwahi pia kutajwa kama one of the Top 10 kwaito legends of
all time by DStv’s MTV Base. anasifika kutengeneza nyimbo kali
zinazo-make headlines hivi sasa, na kusifika zaidi kwenye umahiri wake
mkubwa wa kutengeneza vionjo vya nyimbo ya kuchezeka hivyo kuipa ladha
flani hivi nyimbo, Oskido anafananishwa na David Gueta wa marrekani kwa
umahiri wake katika kupaisha nyimbo na kuifanya ikubalike hata kwa mtu
ambaye hailewi lugha inayotumika kwenye wimbo.Hii ni moja ya kazi ya
Oskido inayo make headlines hivi sasa, akimshirikisha May D.
Post a Comment