Na Baraka Mbolembole
Falsafa ya utilitarianism inasema kuwa njia bora katika maisha ni kutafuta kuridhisha watu wengine kadri iwezekanavyo na kupima vitendo vya watu watu kama kigezo , kila tendo la mwanadamu lazima liongeze furaha kwa binadamu mwingine, katika fainali za kombe la dunia zinazoendelea nchini Brazil mshambulizi wa Uruguay, Luis Suarez tayari ameonesha makali katika ufungaji wa mabao, lakini tukio lake la kung’ata meno mlinzi wa timu ya Italia linaweza kufanya wengi kuamini kuwa mchezaji huyo hajapiga hatua yoyote katika suala la ubinadamu.
Suarez amewahi kufanya vitendo vichafu uwanjani miaka ya karibuni na tukio lake kubwa la mwisho lilikuwa ni kumng’ata meno mchezaji wa Chelsea, Banslav Ivanovic katika mchezo wa ligi kuu England misimu miwili iliyopita. Suarez alifungiwa na Chama cha Soka cha England, FA kushiriki michezo kumi ya ligi hiyo.
Alikosa michezo saba ya mwanzo ya klabu yake ya Liverpool msimu uliopita kama sehemu ya adhabu hiyo. Aliporejea uwanjani alifanya mambo makubwa. Alitwaa tuzo mbili za uchezaji bora wa mwaka nchini England, na aliweka rekodi ya ufungaji wa juu zaidi kwa msimu katika historia ya ligi kuu England.
Suarez alivuta hisia za wapenzi wengi wa soka duniani baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa Uruguay dhidi ya England. Alifunga bao la kuongoza kwa mpira wa kichwa na kuthibitisha kuwa ni mchezaji aliyekamilika na akafunga bao la ushindi mjwishoni mwa mchezo akifuta lile la kusawazisha la Wayne Rooney na kufufua matumaini ya timu iliyofika fainali ya michuano hiyo mwaka 2010.
KIPAJI NA TABIA MBAYA UWANJANI
Suarez alipigana kama ilivyo kawaida yake katika mchezo muhimu dhidi ya Italia siku ya jana. Uruguay ilihitaji ushindi tu ili kufuzu kwa hatua ya 16 bora. Uruguay ilishinda mchezo huo dhidi ya Italia ambao sare tu ingewavusha kwa hatua ya pili. Giorgio Chiellini mlinzi wa kati wa Italia ambaye hucheza mchezo wa nguvu alionekana kumthibiti mshambulizi huyo wa Liverpool katika muda mwingi wa mchezo huo. Na kitendo hicho kilikuwa kama kumpandisha hasira Suarez kumng’ata, Chiellini sehemu ya nyuma ya bega lake bila sababu yoyote.
Uruguay ilipata bao pekee katika dakika ya 81 lililofungwa na mlinzi, Diego Godin dhidi ya timu iliyokuwa pungufu na kucheza soka la kujihamini timu ya Italia ambayo mchezaji wake wa kiungo Claudio Marchisio alioneshwa kadi nyekundu dakika nane kabla ya Suarez kumng’ata Chiellini. Machisio alipewa adhabu stahili, lakini maneno ya mlinzi Chiellini ambaye amelitaka Shirikisho la Soka duniani, FIFA kutoa adhabu kali kwa mchezaji huyo ambaye pia amewahi kufanya matukio kama hayo akiwa katika klabu za Ajax Amsterdam na Liverpool. Licha ya kiwango chake kizuri ndani ya uwanja Suarez ameshindwa kudhibiti matukio yake yasiyo ya kiungwana katika soka.

Uruguay itacheza na Ugiriki siku ya jumapili katika mchezo wa hatua ya mtoano, nafikiri FIFA, wanapaswa kumpatia adhabu mchezaji huyo ambaye alifanya kitendo hicho bila kuonekana na waamuzi wa mchezo huo muhimu. Suarez apewe adhabu kali ili fundisho lingine kwake. Soka ni mchezo wa kiungwana ila Luis Suarez amekosa ubinadamu japokuwa ni mchezaji bora katika kizazi cha sasa duniani.
Post a Comment