0
Mshindi wa tuzo za Oscar, Mkenya Lupita Nyong’o ameungana na waigizaji wengine wa zamani kwenye muendelezo wa filamu za “Star Wars”.
lupita-nyongo-by-tom-munro-for-vogue-italia-february-2014-4
Muigizaji wa series za “Game of Thrones” Gwendoline Christie naye ataungana kwenye “Star Wars: Episode VII,” iliyoanza kurekodiwa mwezi uliopita na itatoka December mwakani. Kulikuwepo na tetesi za siku nyingi kuwa Nyong’o, aliyeshinda tuzo ya muigizaji msaidizi bora wa kike kwenye Academy Award mwezi March kutokana na kuigiza kwenye filamu ya “12 Years a Slave,” ataungana na filamu ya “Star Wars” .


Waigizaji wengine kwenye filamu hiyo ni pamoja na Harrison Ford, Carrie Fisher, Mark Hamill, Anthony Daniels, Peter Mayhew na Kenny Baker

Post a Comment

 
Top