Tofauti na inavyoaminika na wengi kuwa mfumaniwaji huwa mpole, kibao kimebadilika, mfanyakazi wa ndani aliyejulikana kwa jina la Niachie amegeuka mbogo na kumchoma bisibisi bosi wake, Amina ‘Mama Zai’ aliyemfumania akiwa na mumewe aitwaye Amri.
Tukio hilo lilitokea juzikati maeneo ya Mbagala jijini Dar ambako
mama Zai alimwekea mtego mfanyakazi wake huyo wa ndani baada ya kubaini
kuwa alikuwa akitembea na mumewe wakati yeye akiwa kazini.
Akizungumza na mwandishi wetu siku mbili kabla ya tukio, mama Zai alidai kuwa mumewe ana kawaida ya kufanya mapenzi na mfanyakazi wao wa ndani wakati yeye akiwa kazini hivyo akaandaa mtego ili kukomesha tabia hiyo.
Mama Zai alizidi kumwaga data
kuwa, yeye ni nesi katika hospitali moja ya mtu binafsi iliyoko Jangwani
jijini Dar hivyo akiwa zamu ya usiku, mumewe hutumia mwanya huo
kubanjuka na hausigeli.
“Ananivizia nikitoka tu na akijua nimeshafika mbali, anaingia
chumbani kwa hausigeli na kuvunja naye amri ya sita,” alidai mama huyo.
Mama huyo alisema ili kufanikisha
zoezi la kumnasa mumewe, alijifanya anakwenda zamu ya usiku kisha
akajifungia stoo ili aweze kufanya fumanizi matata.
Ilipofika saa tano usiku, baba Zai aliingia katika chumba
cha mfanyakazi huyo kwa lengo la kungonoka naye . Baada ya kuona hivyo, mama Zai
alivamia chumba hicho na purukushani ya
nguvu ikaanza.
Katika harakati za kujinasua katika kipigo cha bosi wake, hausigeli
huyo aliokota bisibisi na kumchoma mama mwenye nyumba shingoni kisha
kutimua mbio huku mume naye akiingia mitini.
Credit: Global publisher
Credit: Global publisher
Post a Comment