0


Mtoto Jeremiah Nyamuhanga (2) mkazi wa Machimbo amekufa baada ya kutumbukia kwenye kisima cha maji karibu na nyumbani kwao.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema, mtoto huyo alitumbukia juzi saa 10 jioni katika eneo la Machimbo, Kitunda, Wilaya ya Ilala.
 
Alisema maiti yake ilikutwa ikielea ndani ya kisima hicho kilicho karibu na nyumba yao. Inasadikiwa mtoto huyo alimtoroka baba yake aliyekuwa kwenye banda la kuku na kwenda kucheza ambapo alitumbukia ndani ya kisima hicho.
 
Maiti ya mtoto huyo amehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na upelelezi unaendelea.

Post a Comment

 
Top