0



Juzi, Nuhu Mziwanda alipost picha kwenye Instagram ikionesha Tattoo aliyochora yenye jina la mpenzi wake Shilole ikiwa imeandikwa ‘ShiShiBaby’.
 
Wengi walihoji kuhusu tattoo hiyo kuwa ni tattoo inayodumu au ni ya kuonesha kwa muda itafutika.
 
Katika  Majibu yake, Mziwanda alieleza kuwa tattoo aliyochora ni ya kudumu katika kipindi chote atakachokuwa duniani na kwamba haitafutika mpaka siku anaingia kaburini.
 
Je, itakuwaje wakiachana (hatuombei iwe hivyo)? Nuh ameeleza kuwa yeye hajali kama wataachana au vipi kwa kuwa Shilole ni mtu muhimu sana kwake na amefanya kwa mapenzi yake.
 
“Nilimwambia labda wewe ndio utakaekuja kunizingua lakini mimi hata siku moja sitakuzingua. Hata kama tukiachana, mimi nimeamua hivyo na nimefanya kwa mapenzi yangu kwa sababu nampenda sana na ni mtu muhimu sana kwangu.”
 

Post a Comment

 
Top