0
Naiminia Tanzania ndiyo habari ya mjini, weekend hii siku ya Jumamosi ndani ya uwanja wa Jamhuri,Mkoani Dodoma wasanii wa fani mbalimbali hapa nchini wameandaa ufunguzi wa kampeni kubwa inayoitwa ‘Naiaminia Tanzania’.Ambayo ni muendelezo wa ile ngoma yao ya miaka 50 ya tanzania, ambayo waliirekodi wasanii 50, wakashuti na video.Msanii wa Bongo Fleva,Mwana FA pamoja na Nikki Wa Pili watatoa speech mbele ya mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Dr. Shein, atakuwepo waziri mkuu mh. Mizengo Pinda pamoja na baraza na la mawaziri, na viongozi mbalimbali.
Kwenye uwanja wa Jamhuri Stadium kuzama itakua free bila mtonyo ili raia wote wapate chakula cha ubongo
kwa watakao kuwa nje ya Dodoma wataweza kuona live tukio zima kupitia
Clouds TV, Star TV, na TBC 1 ,Clouds fm imepiga story na mmoja kati ya watu watakaotoa speech mbele mgeni rasmi, anaitwa mwana fa huyu hapa anatutonya kwa ufupi madini yaliyojaa kwenye hotuba yake, cue in .. clip 1 mwana fa
Kauli mbiu ya kampeni hii ya ‘Naiaminia Tanzania’
“ni uzalendo ndo habari ya mjini”
“kabla hujalalamika chapa kazi”
“soko letu bidhaa zetu
“fungua fikra usitengeneze picha

Post a Comment

 
Top