Eti unene wa wake unawafanya wanaume kuwa na mipango ya kando?
Je ni kweli wake wanaponenepa upita kiasi ndio sababu ya waume zao kuwa na mipango ya kando?
Nchini Kenya mjadala umezuka kwenye mitandao ya
kijamii kufuatia maandishi ya mwanamke mmoja akiwalaumu wanawake wanene
kupita kiasi kwa masaibu yanayowakumba katika ndoa zao.
Njoki Chege aliandika katika gazeti
la Daily Nation Jumapili na kwenye blogu yake kusema kuwa sababu ya
wanaume waliooa kuwa na mipango mingi ya kando ni wake zao kujisahau na
kuwa wanene kupita kiasi.
Amesema wanawake wanapoolewa na kubarikiwa na
watoto , unene huzuka na hapa ndipo Njoki anasema pindi mwanamke
anapoonza kunenepa na kuwa mzito kupita kiasi, waume zao husasau yule
kidosho aliyemfumba macho hata akamuoa.
Anaongeza kusema wanawake hao huzua kila sababu kutofanya mazoezi na wakisema wana shughuli nyingi.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_sC_GoAFG9KdbNFls2ePt2TrR1ARAppmSTh58lDNnYQ6lP8LKGaIyi0D5Fs7lf-lxl1be-hHqgwJCpBbqY8MGu6KSm8NS_ap1TjLmXozHBrJ5AhJ66TS4Iju7nT8p51EUEUbMMeGYJnopPDYuHPIZ0WLGVs7Rb_7_a4KiDxN4pk21zbBf2CfRY128bTUAqZCg=s0-d)
Njoki anasema bora wanawake waendelee kuwa na umbo mdogo ndipo wawapendeze waume wao
Kadhalika anasema wanawake hujipatia majukumu
mengi na kujishughulisha kiasi cha kujisahahu. Wao husema unene
umetokana na kupata mtoto lakini kwa Njoki, hicho ni kisingizio tu.
Waume zao wanapotupa jicho huku na kule na
kujionea wasichana walio na umbo zuri basi huingia kwenye mtego wa
kujiingiza katika zinaa.
Matamshi ya Njoki yamewakera wengi hasa wanawake
na kuzua hisia mseto miongoni mwa watu wengi. Bila shaka aliandika
maoni yake na sisi tunakuuliza tu maoni yako.
Kwa nini swala hili la unene na wembamba ndilo linatumiwa kama kigezo kwa wanaume waliooa kwenda nje ya ndoa?
Je unahisi kama kuna ukweli hapa au Njoki ana matatizo yake mwenyewe? Yeye mwenyewe ni mwembamba.
BBC SWAHILI
Post a Comment