Wanasayansi wanasema kutoa ushuzi ni afya
Kila mmoja wetu kwa wakati fulani huhisi kuvimbiwa na gesi nyingi tumboni. Suluhu ya pekee hapa huwa ni kujamba ili kupunguza gesi hiyo tumboni, Sasa Wanayansi katika chuo kikuu cha
Exeter, nchini Uingereza, wanasema kuwa wamegundua harufu mbaya kama
vile ya kujamba japo inachukiza kwa pua, ina manufaa makubwa kwa afya ya
binadamu.
Wanasayansi hao wanasema kuwa harufu hiyo mbaya inaweza kuwa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo na akili na hata Saratani.
Gesi au harufu mbaya ambayo hutokana na chakula kinachosagwa tumboni mwako inaweza kulinda baadhi ya viungo vya mwili wako.
Ndio! athari ni kile ambacho unakidhania: Eti
watu wanauchukulia utafiti huu kumaanisha kuwa harufu mbaya inayotokana
na mtu kujamba inaweza kuzuia magonjwa fulani mwilini kama vile
Saratani.
Utafiti huo uliochapishwa katika mtandao wa chuo
kikuu cha Exter uligundua kuwa gesi hiyo inayojulikana kama Hydrogen
Sulfide ambayo pia hupatikana katika Mayai yaliyooza, inaweza kuwa
muhimu katika kutibu baadhi ya magonjwa.
"ingawa gesi ya hydrogen sulfide inajulikana
kuwa na harufu mbaya na hupatikana katika Mayai yaliyooza pamoja na
harufu ya mtu kujamba, hutengezwa mwilini na inawezekana kuwa tiba kwa
magonjwa fulani, ''asema Daktari Mark Wood,Profesa wa chuo hicho cha
Exeter.
Gesi hiyo ina athari mbaya ikiwa katika viwango vikubwa , kwa mujibu wa utafiti huo.
Watafiti wanasema licha ya harufu hiyo mbaya ya
kujamba kuchukiza, ina uwezo mkubwa wa kupunguza uwezekenano wa mtu
kupatwa na magonjwa kama vile, Saratani,Kiharusi, mshtuko wa Moyo na
kuumwa na mifupa.
BBC SWAHILI
Post a Comment