LEO July 11 ndo siku ambayo usaili wa kuwatafuta washiriki watakaoiwakilisha Tanzania katika reality show ya Big Brother nchini Afrika Kusini utaanza kufanyika.
Mara nyingi zinapokaribia siku za
usaili mashabiki mbalimbali huweka ubashiri wao wa mastaa ambao
wanadhani wanafaa kwenda kutuwakilisha.
Vanessa Mdee ni miongoni mwa
mastaa mabao walitajwa na baadhi ya watu kuwa anaweza kufaa kama
atawania nafasi hiyo mwaka huu.
Hiki ndicho alichojibu Vanessa kama yuko tayari kuwaridhisha
mashabiki wanaotamani achukue fomu na kushiriki kwenye usaili wa kupata
nafasi hiyo.
“Nasikitika kuwaambia wale wote ambao wangependa kuniona katika nyumba ya Big Brother kwamba haitakaa itokee” Amesema Vee Money na kutaja sababu, “character
yangu haiendani na kukaa kwenye nyumba na watu wengi hivyo, yaani I
will be so defeated yaani ntatoka siku ya tatu afu ntawa disappoint wale
waliokuwa wanapenda niwe pale”.
Licha ya yeye kutokuwa na wazo la kushiriki ila amemtaja mtu anayedhani anaweza kufaa kwa nafasi hiyo.
Raheem Da Prince wa Times FM
“I think Rahim should Try, Rahim da Prince. Rahim I think he
understands a lot about the world halafu pia ana personality he is very
outgoing so nadhani angeweza kufanya vizuri pale”.
Lakini pia amemtaja mtu ambaye hastahili na asiyetakiwa hata kujaribu kuchukua fomu:
“Nadhani mpoki asiende”.LOL!
Usaili wa kuwatafuta wawakilishi wa Tanzania kwenye Big Brother
utafanyika kwa siku mbili kuanzia leo July 11 na July 12 katika hotel
ya New Afrika jijini Dar.
Post a Comment