Shirika la afya duniani, limewaasa wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, kutumia dawa za kupunguza makali ya HIV hata ikiwa hawajaambukizwa HIV.
Shirika hilo linasema kuwa ikiwa wanaume hao
watatumia dawa hizo za kuzuia maambukizi pamoja na kutumia Condom,
huenda ikapunguza maambukizi ya HIV miongoni mwao kwa zaidi ya asilimian
20.
Msemaji wa shirika hilo, alisema kuwa kiwango cha maambukizi miongoni
mwa wanaume wapenzi wa jinsia moja, watu wanaotumia madawa ya kulevya ,
wafungwa na makahaba imeongezeka.
Kikundi hicho cha wanaume ndicho kilichoanza kuambukizwa HIV miaka 33 iliyopita.
Miaka ya zamani dunia ilipoanza kuchukua hatua
dhidi ya maradhi ya ukimwi kutokana na picha zilizokuwa zinatisha za
wagonjwa wa Ukimwi, ripoti ya shirika hilo inasema kizazi cha leo
hakijali sana kuhusu ugonjwa huo hasa kwa sababu kuna dawa za kupunguza
makali.
Kwa mujibu wa WHO, haali hii inatishia juhudi dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo.
Kizazi cha leo kinakabiliwa na hatari ya
kuambukizwa HIV zaidi ya maradufu. Mfano nchini Bangkok, idadi ya
wanaoishi na virusi vya HIV kwa wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia
moja, ni 5.7%.
Katika mapendekezo yake mapya , shirika hilo
linataka wanaume waanze kutumia dawa za kupunguza makali ya HIV kama
njia ya kujikinga kutokana na maambukizi
Credit: BBC
Post a Comment