Ben alifanya hivyo baada ya kuwekeana dau la shilingi 500 na mwenzake miongoni mwa aliopanda nao mlima huo.
Kijana huyo mwenye miaka 18 alipanda mlima huo katika kuchangisha
fedha kusaidia watoto wa kituo cha kulea watoto cha Acorns Children's
Hospice kilichopo jijini Worcester nchini England.
Kwa kupanda mlima huo, Ben alikusanya pauni 600 ila baada ya kuvua
nguo zake na kuweka picha yake mitandaoni alichangisha fedha nyingi
zaidi.
Ben ambaye hujitolea katika kituo hicho alipanda futi 19,341 za Mlima Kilimanjaro kwa siku 9 akiwa na wenzake 7.
Ben ambaye ni mwenyeji wa Kingswinford, England alisema: "Kila mtu
alifurahia kitendo nilichokifanya katika kilele cha Mlima Kilimanjaro na
kuchukua picha zangu.
"Wazazi wangu walipigwa na mshangao mwanzoni, ila walipoona watu
wanazidi kuchangia kwa wingi walinielewa maana nilifanya kitu tofauti."
Post a Comment