Beyonce na mumewe Jay Z wamewasurprise wana ndoa huko
Portofino, Italy baada ya kuingia kanisani na kushuhudia tukio la
kufunga ndoa bila wanandoa hao kufahamu uwepo wa mastaa hao.
Lakini kabla ya kuondoka kanisani hapo, Beyonce alimfuata bibi harusi
kumsalimia na hapo ndipo bibi harusi huyo alionesha kushangaa na
kuonesha furaha ya hali ya juu.
Miezi michache iliyopita, Serema Williams nae alijikuta katikati ya
sherehe ya ndoa akiwa ufukweni na vazi la maeneo hayo na kupiga picha
kadhaa.