Mhudumu wa bar kutoka Ujerumani ameweka rekodi ya dunia kwa kubeba glasses 27 za bia kwa mkupuo kwa mikono miwili aliyojaliwa na Mungu.
Mhudumu huyo aliyetajwa kwa jina la Oliver Struempfel alibeba glasses hizo zilizojaa bia na kuzifanya kuwa na uzito wa Kilogram 62 kisha akatembea nazo umbali wa mita 40 bila kudondondosha wala kumwaga tone.
Video: Mhudumu aweka rekodi ya dunia kwa kubeba glasses 27 za bia kwa mkupuo mikononi bila kumwaga
Struempfel aliweka rekodi hiyo katika shindano maalum la tamasha la beer huko Abensberg linalojulikana kama ‘Gillamoos beer Festival’ baada ya kumshinda mpinzani wake ambaye aliweza kubeba glasses 26.
Nimefanya kazi hapa kwenye biashara ya beer (kama mhudumu) tangu miaka 17 iliyopita, kwa hiyo nina mafunzo mengi.” Amesema Struempfel.

LAANA

 
Top