Home
»
UDAKU
» AISHA MADINDA AFANYIWA KITU MBAYA UARABUNI
MNENGUAJI wa
bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’, Aisha
Ramadhani Mbegu maarufu kama ‘Aisha Madinda’, hivi karibuni anadaiwa
kufanyiwa kitu mbaya baada ya kupokonywa pasipoti na simu zake kisha
kubadilishiwa kazi aliyokusudia kuifanya na kufanywa hausigeli. 
Mnenguaji wa bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’, Aisha Ramadhani Mbegu maarufu kama ‘Aisha Madinda’.Akisimulia mkasa mzima, Mkurugenzi wa Aset, Asha Baraka alisema
Aisha alikwenda nchini Dubai kwa lengo la kufanya shughuli za unenguaji,
lakini aliyempokea alimbadilishia kibao kwa kumnyang’anya kila kitu ili
asipate mawasiliano na baadaye kumfungia kwenye jengo moja na
kumfanyisha kazi za ndani.
Asha anayejulikana pia kama Iron Lady, aliendelea kuweka wazi kuwa
baada ya Aisha kufanyiwa hivyo hakuwa tena na uwezo wa kuwasiliana na
mtu yeyote zaidi ya waliomteka, ila yeye alipata habari hizo baada ya
kuwauliza baadhi ya wasichana wanaofanya kazi huko waliomwambia kuwa
tokea wawepo Dubai hawajawahi kumuona wala kusikia habari zake.
“Yaani walimpokonya hati za kusafiria, wakampeleka kufanya kazi za
ndani katika majumba ya watu, nimeshamfuatilia kujua alipo na sasa
tunafanya utaratibu wa kumrejesha nyumbani, inahitajika kama dola 800
(zaidi ya milioni 1)kwa ajili ya kulipia kibali cha kuishi alichokuwa
amepitiliza,” alisema Asha Baraka.
Aisha aliondoka nchini hivi karibuni kwenda huko kwa ahadi ya kwenda
kunengua katika kumbi mbalimbali za starehe, lakini ndoto zake
zikayeyuka.
Tunazani ungependa kusoma hizi