Akiongea na mwandishi wetu, Dk. Cheni alisema yeye hajawahi
kumuomba msanii rushwa ya ngono, isipokuwa anaamini walio wengi
huanzisha mahusiano yaliyo rasmi kwa makubaliano yao kutokana na hisia
zinavyowasukuma.
“Sizani kama ni rushwa ya ngono, naamini wengi wanakubaliana, sehemu
ya watu wengi mnapokutana inatokea watu kupendana na kuwa wapenzi hilo
nakubali sababu ni jambo la kawaida hata wasanii kwa wasanii kupendana,
sidhani kama mtu anaweza kulazimishwa kufanya mapenzi ili acheze filamu,
mpaka watu kufanya tendo hilo wameshakubaliana,” alisema Dk. Cheni.

Post a Comment