Home
»
WANAWAKE
» Madai Mazito: Mchungaji atorosha mke wa mtu
Mchungaji anayejiita nabii na mtume, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) aliyetajwa kwa jina moja la Emmanuel amejikuta ndani ya majanga kufuatia madai mazito kwamba amemtorosha mke wa mtu ambaye ni mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bongo anayekuja juu kwa kasi, Janet Mrema.

Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bongo anayekuja juu kwa kasi, Janet Mrema anayedaiwa kutoroshwa na mchungaji huyo.**********
Kwa mujibu wa chanzo makini, mchungaji huyo alifika nyumbani kwa
Jonas Mrema, mume wa Janet, maeneo ya Tegeta-Nyaishozi jijini Dar na
kuishi kama mtumishi wa Mungu lakini polepole alianza mazoea tata na
Janet.
“Mume alianza kuhisi mabadiliko ya mkewe kwa mtumishi huyo, lakini
nadhani aliona ni mawazo yake tu. Ndipo siku ya siku akashangaa mkewe na
mchungaji huyo wameondoka nyumbani hapo.
“Kwa sasa tangu tukio hilo litokee ni miezi kama mitatu. Mume
alihangaika sana kumtafuta mkewe hadi jana (Jumatatu iliyopita) ndipo
akampata wakiwa na mchungaji huyo kwenye nyumba moja ambako walikuwa
wakiishi pamoja,” kilisema chanzo chetu.
Iliidaiwa kwamba, mchungaji huyo alipopekuliwa alikutwa na paspoti ya
nchini Burundi wakati yeye ni Mkongo wa Uvira na alionekana kuishi
nchini kinyume na sheria hivyo alifunguliwa jalada la kesi kwenye Kituo
cha Polisi cha Wazo Hili, Tegeta lenye Kumbukumbu Na. WH/RB/7040/2014- KUISHI NCHINI BILA KIBALI.
Juzi, Amani liliwasiliana na Katibu wa Chama cha Waimba Injili
Tanzania, Stela Joel ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema
tayari chama hicho kimemsimamisha uanachana Janet kwa kitendo chake
hicho cha kumtoroka mumewe wa ndoa.
“Ni kweli na Chama cha Waimba Injili Tanzania kimemsimamisha
uanachama Janet. Hatuna mzaha katika maadili,” alisema Stela.
Amani
lilimpigia simu mume wa Janet, Jonas Mrema ambapo katika mazungumzo
baada ya salamu alipewa pole kwa matatizo ya mkewe, alisema asante kisha
alipoulizwa kuhusu hali ilivyo aliomba apige simu yeye baadaye kwa vile
alikuwa kikaoni.
Hata hivyo, baada ya saa mbili kupita bila kupiga, Amani lilimpigia
tena simu ambapo iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kumpata
zinaendelea.
Chanzo: Gazeti la Amani/Gpl