Mwanadada Moza Kassim mwanafunzi wa chuo cha Uhasibu
Tawi la Singida, inadaiwa kuwa usiku wa ijumaa kuamkia jumamosi
iliyopita mkoani Singida, alijibizana na mpenzi wake ambaye eti
aligundua kuwa ana mpenzi mwingine na katika vuta ni kuvute hawakufikia
muafaka ndipo mwanadada akamwambia mpenzi wake kuwa anajichoma kisu
mwanaume akajua ni utani akamjibu huwezi, mwanadada akamwambia kwa
mara
ya pili kisha Moza akajipiga kisu tumboni karibu na kiuno hali yake
ikawa mbaya na kuanza kuchuruzika damu ikabidi rafiki zao waliokua
karibu wakamkimbiza hospitali ya mkoa, na jana alihamishwa hospitalini
hapo na mwanadada huyo yupo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi, na kwa
mujibu wa sheria Moza ana kesi ya kujibu.