Moja,
Kuna jirani yetu ana duka, mke wangu akapata story kuwa yule mama na
mumewe ni waathirika. Mwenzangu akatangaza marufuku kwenda kununua kitu
chochote pale. Nikamweleza kuwa kama ukimwi ungekuwa unaambukizwa kwa
style hiyo basi sijui kama kuna binadamu angebaki hapa duniani.
Akaninunia.
Lingine
linalofanana na hilo: Kuna siku alikuja akanisimulia habari za mama
mwingine mwenye duka pale gengeni a.k.a. Mama J ambaye hana mume alivyo
na tabia mbaya, Kuwa anawaingiza wanaume kwake anawabadilisha tu.
Sikutaka kupoteza muda kwenye huo mjadala, kumbe yeye alitaka atoe
ultimatum kuwa ni marufuku kwenda kununua bidhaa kwenye hilo duka. Siku
moja akaniomba nimsindikize tukachukue maziwa mida ya jioni kwani mwenye
kuuza hakuweza kuleta. Wakati huo, tulikuwa tunatafuta mayai ya
kienyeji na upatikanaji wake ni wa shida.
Sasa tukiwa tunapita barabarani nikaona kwa duka la mama J ana mayai ya
kienyeji tena mengi tuu. Saa ya kurudi nikashauri tuchukue mayai,
akasema twende nyumbani. Nikamshawishi kwani upatikanaji wa mayai ni
shida, tukapitia pale tukachukua mayai kumi. Pia nikanunua vocha ya
tigo. Mama J akasema vocha iliyobaki ni ya kurusha. Nikamwambia poa
nirushie, nikamtajia namba. Kumbe hapo ndo nikawa nimetibua nyongo bila
kujua.
Tulipotoka
pale njia nzima nikaona mtu kanuna hataki kuongea. Kufika home kaniita
chumbani akaanza kunigombeza, eti mbona alishaniambia tabia za yule mama
alafu bado naenda kununua vitu kwake?
Pili,
nikipigiwa simu haijalishi ni muda gani na ni wapi, lazima aulize nani
amekupigia na anasemaje. Ukweli hata nikimwambia hawezi kumfahamu kila
mtu na siyo kila kitu naweza kumsimulia, mambo mengine ni ya kikazi.
Kila wakati anapekua simu yangu kana kwamba niko polisi.
Tatu,
tumebahatika kuwa na usafiri, na tunapokaa daladala ni za shida kidogo.
Hivyo, kila asubuhi lazima tutoke wote, tumpitishe mtoto shule, then
nimdrop yeye kazini. Sasa tukiwa njiani akimwona mtu yeyote anayemfahamu
ananiamrisha tumpe lifti huyo mtu. Kumbuka mimi simwulizi kuwa huyo mtu
ni nani wake. Nachukulia kawaida. Sasa ikitokea mimi nimemkuta mtu
ninayemfahamu au rafiki yangu, huyo mtu akishuka kwenye gari, basi
nitaulizwa maswali kama vile niko polisi nahojiwa. Na bahati mbaya ikiwa
ni mwanamke, basi ananuna na wakati mwingine nikitaka kusimama anasema
twende bana tunachelewa. Hii imenikera sana kuliko kawaida.
Sasa,
kuna shosti zake wa karibu sana, mara nyingi nawapa lifti anapotoka
kazini, basi anawasifia sana kuwa wana tabia nzuri, sometimes ananiomba
tuwapeleke mpaka mjini japo sina ratiba ya kwenda huko. Sasa hao
mashosti zake nimetembea nao na hajui. I just wanted to prove kuwa mambo
yake ya kijinga hayanizuii kufanya nikiamua. Jamani kumlinda mpenzi ni
sawa na kulinda samaki baharini, ukilinda Kigamboni wenzako wanavua
bagamoyo.
Anyway, nipeni wazo mbadala nimfanyeje ili aelewe hilo somo?
Post a Comment