Kwa mujibu wa Bigeye ya Uganda, Luzinda amewaambia marafiki zake jinsi alivyokuwa maarufu kupitia picha moja tu ya utupu.
“Nimepoteza muda mwingi kufanya muziki, nimejitahidi sana kutoa
hits. Yote hiyo ilikuwa kazi ngumu, lakini picha moja tu ya utupu Uganda
nzima inanizungumzia mimi. Nimeweza hata kwenda BBC na Daily Mail.
Muziki wangu usingeweza kunifikisha kwenye hizo sehemu lakini mwili
wangu umeweza.” Inadaiwa Luzinda aliwaambia marafiki zake.
Aliongeza, “Nafikiria mtu kama Kim Kardashian anaogopa kwasasa.
Vinginevyo, kwanini akimbilie kupiga picha za utupu wakati ambao BBC
imenihoji mimi. Anahofia. Hataki kukubali ukweli kwamba sisi watu weusi
tuna miili mizuri na tunavutia. Kama yeye ame ‘break the Internet, mimi
nitaivunja vizuri zaidi.”
“Kuna vingi tunavyofanana, lakini lazima niseme, mimi ni mzuri
zaidi, Wakati ambapo mkanda wangu wa ngono utakapotoka, mkanda wa ngono
wa Kim utapotea kwasababu wangu umejaa mvua za elnino. Lakini ngoja
niende taratibu, muda ukifika, sitavunja tu internet, nitaifunga
internet na ‘bombastic s3xtape’ yangu.”
Wakati huo huo Luzinda ameingia studio kurekodi wimbo uitwao
‘Apology’, ukiwa ni maalum kwaajili ya kuwaomba radhi mashabiki wake,
marafiki na familia.
Post a Comment