Elizabeth Michael ‘Lulu’ akipozi..
Elizabeth Michael
‘Lulu’ amefunguka kuwa kamwe hapendi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi
na masharobaro akidai kuwa siku zote ni pasua kichwa ila anazimikia watu
wazima waliomzidi sana umri.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Lulu alisema akiwa na
mwanaume anapenda ampite angalau miaka kumi na kuendelea kwa kuwa
anakuwa ni mtu mzima na muelewa siyo masharobaro kila wakati wanafikiria
jinsi gani wataonekana smati na si kufikiria maisha.
“Masharobaro hawana nafasi kwangu, kwa sababu hawafikirii maisha
kabisa, hata mwanaume atakayenioa nafikiri atanipita zaidi ya miaka
kumi, hapo ndiyo itakuwa sawa tofauti na hivyo sitaki masharobaro,”
alisema Lulu.
Post a Comment