Awali,
Novemba 11, mkulima Hassan Kondeja mkazi wa Kitongoji cha Bwawani Kijiji
cha Matui aliuawa kwa kukatwa shingo na wafugaji na ndipo yakatokea
mauaji ya wakulima wawili na wafugaji wawili.
Akizungumza
na mwandishi wetu, Kamanda wa polisi wa Mkoa Manyara, SACP Deusdedit
Nsimeki alisema wakulima wawili wameuawa jana kwa kukatwa na mapanga na
watu wanaodaiwa kuwa ni wafugaji wa jamii ya Kimasai.
Kamanda
Nsimeki aliwataja wakulima hao waliouawa ni Juma Omary (65) na Nyanya
Ngoroka (70) wote wakazi wa Kijiji cha Cheka Nao, kata ya Kiperesa
iliyopo mpakani na wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
“Chanzo
cha mauaji hayo ni ugomvi uliotokea kati ya wafugaji kuingiza mifugo
yao kwenye shamba la wakulima hao na walipowakataza wakatumia silaha za
moto na kuwakata mapanga wakafa papo hapo,” alisema Kamanda Nsimeki.
Alisema
vifo hivyo vinatokana na kulipiza kisasi kati ya wafugaji na wakulima
ambao chanzo chake ni migogoro ya ardhi ya muda mrefu.
Naye,
mkuu wa mkoa huo, Elaston Mbwilo alisema wapo baadhi ya viongozi
wamekuwa wazembe hawawajibiki katika nafasi zao na kuwa sehemu ya baadhi
ya migogoro inayoendelea Kiteto.
Aliyasema hayo mjini
Kibaya akizungumza na wazee maarufu wa jamii ya wafugaji na wakulima,
ili kujua kiini cha mauaji yaliyotokea Matui ambapo watu watano waliuawa
kwa kukatwa mapanga.
Mbwilo alisema wapo baadhi ya viongozi kuanzia ngazi ya Kata,Vijiji na Mitaa wamebeba uongozi bila kujua dhamana zao.
Post a Comment