ALIYEKUWA
mchumba wa msanii wa filamu Bongo, marehemu Sheila Haule ‘Recho’,
George Saguda amefunguka kuwa picha za mwanadada huyo zimekuwa
zikimfanya asiwe na hisia za kuwa na mwanamke mwingine.
George Saguda akiwa na aliyekuwa mchumba wake marehemu Sheila Haule ‘Recho’.
Akipiga stori na gazeti hili hivi karibuni, Saguda alisema tangu
mchumba wake huyo afariki dunia hajawahi kuwa na mwanamke na hana mpango
huo kwa sasa labda hapo baadaye.
“Tangu alipofariki Recho niko peke yangu na sina mpango wa kuwa na
mwanamke mwingine, kwani kila ninapozitazama picha zake naumia sana,”
alisema Saguda.
Saguda aliongeza kuwa, licha ya kwamba yeye ni mwanaume
aliyekamilika lakini tangu mchumba wake alipofariki dunia hana hisia za
kimapenzi kwa mwanamke mwingine na akipata hali hiyo huzitazama picha
zake hisia hizo hutoweka.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.