Kama
hujui hii ndio list ya mastaa wa kike watano wanaofanya muziki
walioongoza kwa kuingiza mkwanja mkubwa kwa kipindi cha mwaka 2013-14
Marekani.
No.1- Beyonce:
Mauzo ya Albam yake aliyoitoa kwa sapraiz mwaka 2013, mkwanja
alioukusanya katika show zake unakadiriwa kuwa dola bil. 2.4 kwa show ya
jiji moja, na hesabu zimeonyesha ameingiza jumla ya dola milioni 115 na
kuwa mwanamuziki aliyezalisha pesa nyingi zaidi kwa mwaka 2014.
No.2- Taylor Swift:
Huyu ni msanii wa kike pekee ambaye mauzo yake yanaweza kugonga
platinum kwa mwaka huu, na akikusanya na pato lake kwenye mfuko wa
kutangaza bidhaa, anakuwa na jumla ya dola milioni 64 mwaka huu.
No. 3- Pink:
Huenda asiwe moja kati ya maarufu waliotawala mainstream, lakini lundo
la cash anayoikusanya ‘kimyakimya’ inafikia kiasi cha dola milioni 52
kupitia show zaidi ya 85 ambazo zimemuingizia kama dola mil. 1 kwa kila
show, na kitita kingine safi akijipatia kupitia madili yake ya matangazo
ya bidhaa.
No. 4- Rihanna:
Dada lao amekunja mkoba wa kushiba kupitia madili anayofanya na
makampuni mbalimbali ya fashion, pamoja na kitita alichokikusanya kwenye
tour aliyofanya na Eminem, mwaka huu hajaingiza albamu sokoni kwa hiyo
kumbe bila kuimba muziki bado Rihanna anaweza kuzalisha pesa nyingi
kutoka upande mwingine.
No. 5- Katy Perry:
mkali wa rekodi ya “Dark Horse”, mauzo ya tiketi za show zake sehemu
mbalimbali duniani, na mkwanja wa deal za matangazo umemfanya akusanye
jumla ya kiasi cha dola mil. 40.
Wapo mastaa ambao wana majina ambayo yanasikika sana kama Nick Minaj
hawajaweza kuingia hata kwenye top five ya wale walioingiza mkwanja
mkubwa mwaka huu.
Post a Comment