0
Ray J Jumatano  jana alipiga simu 911 kwa wasiwasi na kumwambia aliyepokea kuwa mpenzi wake ametishia kujiua.

Ray J and Princes Love

Kulingana na vyanzo vyetu, Ray J aliamua kuvunja mahusiano na mpenzi wake Princess siku ya Jumanne usiku. Chanzo kinasema mwanadada huyo aliendelea kumtumia mesegi za kimapenzi Ray J asubuhi yake akiwa kazini. Princes alipokosa kusikia alichohitaji kusikia ndio akaanza kutoa vitisho hivyo vya kutaka kujiua.

Ray J na Princes kabla hawajatemana

Inasemekana RayJ alijua kuwa kuna bunduki ndani ya mjengo wa mdada huyo hivyo alichukulia tishia hilo kwa umakini. Ray J alibainisha kwa aliyepokea simu 911, kuwa rafiki yao mzuri Earl Hayes alijiua mwenyewe hivyo kumtia mtu wa 911 katika tahadhari ya juu.

Polisi walienda hadi nyumbani kwa Princes lakini hakuwepo nyumbani. Polisi hawakuongea naye lakini Ray J sasa anasema yeye tu alizungumza naye na yeye anasisitiza kuwa hatokamilisha hilo tishio.

Post a Comment

 
Top