Home
»
KIMATAIFA
» SI MAAJABU NI KWELI, KUTANA NA SANAMU LINALOISHI
Kwa masaa nane, siku tano za wiki, Paul Edmeades a.k.a ‘Golden Man’huvumilia maumivu ya mwili na misuli, kusengenywa na hata mara nyingine kupigwa ngumi au kusukumwa yote ikiwa kama sehemu ya utafutaji wake wa kipato.
|
'Golden man akiwa amesimama na mwandishi wa habari. |
Ameshatemewa mate, ameshakaliwa na wapita njia na hata kunuswa na mbwa wanaompita barabarani. na hata ndege hutua juu ya kichwa chake na mara nyingine mbwa au paka wanaodhurura hulala kando ya miguu yake. Cha kushangaza ni kuwa 'golden man' mwenyewe hufurahia yote haya kwani kwake ni ishara kuwa anachokifanya anakifanya vizuri kwa umakini mkubwa.
|
Mpita njia akiishangaa sanamu hiyo hai |
Kwa ufupi Paul ni moja kati ya aina nyingi ya sanamu zinazoishi. sanamu hizi ni watu ambao hujivika au kuipaka vitu vyenye rangi ya silver na kisha kusimama kwa utulivu mkubwa kando ya barabara kaita maeneo yenye watu wengi.
|
Watu walijiweka kwenye mionekano ya kisanamu |
'Golden Man' yeye hujipaka rangi ya gold na huvaa suti yake yenye rangi ya gold na kisha husimama katika south bank ya London
|
Paul akiwa kazini
|
Ukijumuisha na kipande cha chuma ambacho hukiweka chini ambacho kimeungana na kikalio ambcho hukificha ndani ya suti na hivyo kumsaidia kukaa kwenye misimamo hii inayopingana na science ya mvuto wa dunia
|
Moja ya watu wanaojipatia kipato kwa njia hii |
Post a Comment