
Maafisa waandamizi wa ulinzi
nchini Malaysia wametoa maelezo kuhusu msako unaoendelea katika bahari
ya kusini ya Uchina kuitafuta ndege ya Shirika la ndege la Malaysia
iliyopotea.
Mkuu wa jeshi la Malaysia - Jenerali Zulkifeli
Mohd Zin - aliwaambia waandishi wa habari mjini Kuala Lumpur kwamba meli
na ndege nyingi zinatumiwa katika maeneo mawili ambapo ndege hiyo
inaweza kuwa ilianguka.Data ya radar imeonesha kuwa pengine ndege hiyo iligeuza njia na kujaribu kurudi Malaysia.
Na msemaji wa Shirikala Ndege la Malaysia amewaambia jamaa wa watu waliokuwamo ndani ya ndege hiyo kwamba wajitayarishe kuwa habari zinaweza kuwa mbaya.
Alisema hakuna mawasiliano na ndege hiyo kwa zaidi ya saa 30 sasa.
Mume wa Danika Weeks alikuwamo kwenye ndege hiyo.
Bado anasubiri kabla ya kuwaambia watoto wake yaliyotokea:
"Siwezi kutazama mbali.
Nashughulika na ya dakika moja tu ijayo.
Nina watoto wadogo wawili na mmoja wa miaka mitatu ambaye ananiuliza "baba atapiga simu ya Skype saa ngapi?'
Ana ramani ukutani, baba ake alimuonesha anakokwenda..
Kwa hivo unajua tena, ananiuliza baba ashafika alikokwenda, lini atapiga simu?
Bahati nzuri hivi sasa yuko na marafiki zake.
Nitawaeleza wakati ukifika..
Yaani ikiwa ndio lazima."
Post a Comment