Staa huyo wa Sinema ya Devil Kingdom ya mwigizaji Emmanuel Myamba ‘Pastor Myamba’ alifunga ndoa hiyo Ijumaa iliyopita kwenye Msikiti wa Mbezi, Tanki-Bovu, Dar na kufuatiwa na bonge la sherehe katika Ukumbi wa Mbezi Beach Park.
Katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa na wanahabari wetu, ilipambwa na watu mbalimbali wakiwemo mastaa wa filamu za Kibongo.
Shughuli hiyo ya kukata na shoka iliwashangaza watu kutokana na maharusi hao majina ya baba zao kufanana huku wageni waalikwa wakisema kwamba ikitokea hivyo ndoa huwa inadumu kwa muda mrefu.
Akizungumza mbele ya wageni waalikwa, Aki wa Bongo Muvi alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa ametimiza ahadi ya ndoa kwani mara ya kwanza walikutana na mkewe kwenye Chuo cha TFTC cha Pastor Muyamba na kuanzisha urafiki hadi wakafikia hatua hiyo ya ndoa.
“Namshukuru sana Pastor Muyamba kwani ndiye mwalimu wangu wa sanaa na kama siyo sanaa, nisingempata mwanamke kama huyu, yaani siku ya leo nina furaha sana,” alisema Aki wa Bongo Muvi ambaye ameandika historia kwa tukio hilo.
Baadhi ya wasanii waliohudhuria kwenye sherehe hiyo ni Pastor Muyamba, Zawadi, Nova ambaye alikuwa mshehereshaji na Rais wa Shirikisho la Filamu la Tanzani (TAFF), Saimon Mwakifwamba ambaye aliwapongeza kwa hatua hiyo ya kuingia kwenye ndoa huku akiwataka wasanii wengine kuiga mfano wao.
Baadhi ya sinema alizoigiza Aki wa Bongo Muvi aliyezidiwa urefu kiaina na mkewe ni pamoja na The Lost Sons, Sometime Yes, Sometime No, Yes Madam, Devil Kingdom, Pastor Muyamba Temptation, Uncle Mpozemenye na nyingine
Post a Comment