Baadhi ya wasanii wa filamu akiwemo Yobnesh Yusuphn(Batuli),Bondi Bin Salim aka Bond, Deogratius Shija na Kulwa Kikumba ‘Dude’wameelezea jinsi walivyopokea kwa uchungu taarifa za kifo cha msanii mwenzao Adam Kumbiana aliyefariki dunia leo.
Wakizungumza na mtandao huu, wasanii hao kwa nyakati tofauti tofauti
kila mmoja ameonesha kuguswa na taarifa hiyo huku kila mmoja akielezea
jinsi alivyopokea taarifa hizo kwa majonzi makubwa.
Dude
“Adam Kuambiana amefariki kweli,chanzo hakijajulikana zaidi lakini kwa
taarifa tulizozipata mwanzo inasemekana asubuhi alijisikia vibaya akaona
kama mwili unaishiwa nguvu hivi,kwahiyo watu wakachukua gari kumpelea
hospitali ndo akafia kwenye gari. Nawapigia sasa hivi simu Mtitu na
Stive Nyerere wanaupeleka mwili hospital, wengi wanasema alianza usiku
vidonda vya tumbo.”
Batuli
“Msiba unauma sana, ghafla halafu kijana,inauma sana ninachoweza kuongea
kwa sasa hivi, ni swala moja kwanza kukubali matokeo la pili ni
kumuombea, ameondoka na sisi tunafuata.”
Bondi
“Kweli na mimi nimesikia hivyo, Adam Kuambiana amefariki akiwa location
mitaa ya Sinza, kwahiyo msiba tumeupokea kwa huzuni kubwa ila tumuombee
kwa mungu.”
Deogratius Shija
“Nimesikitishwa na kifo cha Adam Kuambiana,lakini pengo la Adam Kuambia
ni kubwa sana, jamaaa alikuwa jembe kwenye filamu, unajua imekuwa ghafla
labda ata angeumwa lakini duh ndiyo hivyo hakuna jinsi tumuachie
mungu.”
Post a Comment