Aunt Ezekiel amepitia maisha magumu sana kabla
ya kufika alipo leo. Ili kujua maisha yake halisi ungana na mimi, Imelda Mtema.
Mwandishi: Mambo Aunt? Natumaini uko mzima. Mimi ningependa kujua zaidi historia ya maisha yako kuanzia ulikotokea hadi ulipo sasa.
Aunt: Duu! Sawasawa! Mimi nimezaliwa mwaka 1988 hapahapa jijini Dar es Salaam. Ni mtoto wa pili kwa mama yangu mzazi kwa sababu kwa baba nina ndugu zangu wengine.
Mwandishi: Kwa hiyo una maanisha kabla ya baba yako kuwa na mama yako alikuwa na mwanamke mwingine?
Aunt: Ndiyo.
Mwandishi: Wakati huo ulikuwa ukiishi hapa Dar es Salaam sehemu gani?
Aunt: Nilikuwa nikiishi Ilala na nilipata elimu yangu ya msingi katika Shule ya Msingi Bunge mwaka 1995 mpaka 1998, nikaenda kumalizia Kisarawe, Pwani.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.