0


Aliyekuwa muwakilishi wa Kenya kwenye Big Brother Africa The Chase mrembo Huddah Monroe ambaye mwaka huu anaonekana kuwa kimya kidogo na kuoenesha utulivu tofauti na ilivyokuwa mwaka jana amewachapa bakora ya maneno watu wake wa karibu.

Huddah

Huddah amewashambulia watu wake wa karibu kwa madai kuwa wao ndio wanaozunguka sasa hivi kwenye mitandao wakisema kuwa amefulia na hana kitu tena.

“Kama viatu vinakutosha, vaa!…. nimetambua watu wanaonizunguka wanafanya maisha yangu kuwa magumu zaidi na wanafanya nionekane kama mwehu kwa sababu watu huamini wanachosema! Tetesi zote hizi zinazosambaa, oh Huddah amefulia, Huddah anatumia madawa, Huddah yuko hivi na vile, so what??? Hamfahamu nakotoka, hamjui naelekea wapi. Hasa hawa wanaoitwa sijui Mameneja wa hii dunia ni wasaliti (Snitches) wabaya zaidi! Mother F***es huifanyii kazi lakini wanataka kushare na wewe ulichokihangaikia, hata hawabishi hodi milangoni kukupa kazi halafu wanakimbia huku na kule kumwambia kila mtu eti umefulia. Hell yeah, nimefulia kwa sababu siwalipii vitu kwa uvivu wenu! Nyie wote mnaweza kuzunguka mkawaambia watu jinsi ambavyo Huddah hawezi kumlipa mameneja wake! Mimi nitakaa hapa na kufurahia maisha yangu ya utajiri/kufulia!

Post a Comment

 
Top