Viongozi hao wawili walikutana na Papa nje ya nyumba yake, kabla ya kusafiri pamoja naye na kiongozi wa kanisa la Orthodox, Askofu Mkuu Bartholomew, hadi kwenye sherehe katika bustani ya Vatikani.
Wakitarajiwa kupandisha mzaituni kama alama ya kudumu ya hamu ya pande zote mbili ya kupata amani baina ya watu wa Israil na Palestina.
Papa alisema yeye hataki kuhusika moja-kwa-moja na mazungumzo ya amani, lakini anatumai viongozi hao wakikutana, huenda ikasaidia kupunguza uhasama kati yao.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.