Mariah Carey na mumewe Nick Cannon wanaweza kuachana hivi karibuni kama hawataweza kushinda jaribu la michepuko linaloitikisa ndoa yao.
“Nick Cannon haishi nyumbani kwao hivi sasa, anaishi hotelini. Wanagombana sana.” Kimesema chanzo kimoja.
Chanzo kingine kimeeleza kuwa Mariah Carey amechoshwa na tabia za Nick Cannon kuwa na michepuko mingi kiasi kwamba aliwatuma walinzi kumuangalia akae mbali na warembo wakati wa pool party iliyofanyika Las Vegas ambapo mumewe alikuwa mshereheshaji.
Mariah hakutaka kabisa mumewe anywe pombe katika party hiyo kwa kuwa alijua huingia katika matatizo baada ya kunywa.
Mariah na Nick walifunga ndoa mwaka 2008
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.