0

Mwanamitindo raia wa Sudan aishie Marekani, Ataui Deng aliyepotea kwa muda wa wiki mbili huku akitafutwa na polisi amekutwa akiwa hai katika hospitali moja nchini humo.
Marafiki wa mwanamitindo huyo walitoa taarifa polisi na kuanzisha kampeni maalum ya kumtafuta baada ya kushindwa kumpata kwa kipindi kirefu, kampeni ambayo iliungwa mkono na watu maarufu akiwemo Rihanna.
“Kama mtu yoyote ameshapata taarifa kuhusu alipo huyo binti mdogo, tafadhali wapigie kitengo cha polisi cha Newyork (NYPD) au tuma barua pepe findataui@gmail.com.” Ilieleza tweet ya Rihanna.

Boyfriend wake, Grand Monohon alisema kuwa mara ya mwisho alimwambia kuwa anaaka kwenda mbali lakini aliacha simu na kila kitu chake nyumbani kwao.
Hakuna taarifa rasmi zilizotolewa  kuhusu hali ya Autui hadi sasa.
Kwa mujibu wa polisi, Ataui aliyeingia nchini Marekani kama mkimbizi akitokea kwao Sudan, alionekana kwa mara ya mwisho August, 6 majira ya saa tano usiku.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

LAANA

 
Top