Demu aliyetoka kwenye mahusiano
Kwanini atazingua : “mademu walitoka kwenye mahusiano wanavutia sana, kwasababu wamejawa na shauku lakini ukweli ni kwamba wanasambaratisha moyo wako” , amesema Donna Barnes , mtaalamu wa mahusiano. Demu aliyoachwa anatafuta njia ya kuepuka huzuni kupitia wewe. Demu aliyeachwa hawezi kukaa peke yake na atatafuta mtu yoyote atakayemfanya ajisikie vizuri.Na pia ni rahisi kuhusisha matatizo ya mahusiano yake yaliyovunjika na mahusiano yako.Demu anayechukia kazi yake
Kuna mademu kibao hapa mjini ambao wanachukulia poa kazi zao kwasababu hawajisikii kufanya kazi na wanatafuta mtu anayeweza kuwasaidia.
”Mademu wengine wanaweza kua wanatafuta wanaume kwa sababu mbaya kama account yako ya bank” , anasema Rachel Sussman mwandishi wa kitabu cha “The Breakup Bible.” aliendelea kwa kusema kama mwanamke anahama kazi kila saa au anasema kwamba hataki kufanya kazi basi jua anategea pesa zako.
“Washkaji wengi hupenda mademu wanaokunywa kwasababu wanaonekana kua na mzuka sana” anasema Sussman , lakini ni vizuri kuendelea nae kunywa kwa umakini. Wengi hunywa kwasababu ana siku mbaya au kaachwa na wanawake wengi hua wenye hisia kali pindi wanapokua wamekunywa.Kwa namna nyingne usiku uliyofikiria unaweza kua na mzuka unaweza kubadilika na kua usiku wa mtu kujiliza tu…
Kama kila story anayopiga inahusu kitu kibaya kilichotokea na katika story zote yeye yakua na kosa basi inabidi uogope . Mtu kama huyu hawezi kujichukulia majukumu kwahiyo hamna kosa linaloweza kua lake na hawezi kuona nia ya kubadilisha tabia yake. Watu wengi hulalamika sababu hawana kitu cha kuzungumza , kwahiyo kama unakutana na demu siku ya kwanza na kila story inahusisha watu kumharibia na malalamiko basi bora ukakimbia mapema.
Kama kila saa yupo na smartphone yake hii inamaanisha anahitaji kuwasiliana na watu kila saa ili asijione mpweke.Kama haongei na rafiki zake basi yupo na mambo ya ofisini.Kama mtu anashindwa ka mfano kuachana na mambo ya kazini siku ya ijumaa usiku basi hii inaweza kuwa tabu baadae.
Post a Comment