Beki wa pembeni wa klabu ya Tottenham Hotspurs ambae msimu uliopita
alipelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya QPR, Benoît Pierre David
Assou-Ekotto, usiku wa kuamkia hii leo alionyesha kitendo cha utovu wa
nidhamu ambacho hakikuwafurahisha mashabiki wa soka duniani kote.
Assou-Ekotto na Benjamin Moukandjo
Assou-Ekotto, ambae alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya
Cameroon alidiriki kumpiga kichwa mchezaji mwenzake Benjamin Moukandjo
baada ya malumbano yaliyoibuka kati ya wawili hao, kufuatia kichapo cha
mabao manne kwa sifuri walichokipokea kutoka kwa Croatia.
Hata hivyo hasira za beki huyo mwenye umri wa miaka 30, hazikuishia
uwanjani, bali zilizoendelea hadi nje ya uwanja kwa kulumbana na
Moukandjo, lakini nahodha na mshambuliaji wa Cameroon, Samuel Eto’o
aliingia kati na kujitahidi kuzituliza hasira za Ekotto.

Kitendo
kingine cha utovu wa nidhamu kilichojitokeza wakati wa mchezo wa jana,
ambao ulishuhudia Cameroon wakiambulia kichapo cha pili mfululizo katika
michezo ya kundi la kwanza, ni baada ya kiungo wa FC Barcelona
Alexandre Dimitri Song Billong, kumpiga kiwiko mgongoni mshambuliaji wa
Croatia Mario Mandžukić.
Kwa matokeo ya kufungwa mabao manne kwa sifuri, timu ya taifa ya
Cameroon imeondolewa katika kinyang’anyiro cha fainali za kombe la dunia
za mwaka huu, licha ya kusaliwa na mchezo mmoja dhidi ya wenyeji Brazil
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.