0
Mshambuliaji wa timu ya Uruguay, Luis Suarez akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 39 kipindi cha kwanza.
Luis Suarez akipiga mpira kichwa kufunga bao la kwanza.
Wachezaji wa timu ya England wakiwania mpira.
Rooney akishangilia baada ya kuifungia bao lililokuwa la kusawazisha England.
Rooney akipiga shuti kufunga bao la kusawazisha dakika ya 75.
Mshambuliaji wa timu ya Uruguay, Luis Suarez, akishangilia baada ya kufunga bao la pili dakika ya 85.
Wachezaj wa timu ya Uruguay wakishangilia kwa kumpongeza Luis Suarez kufunga bao la ushindi.
Kocha Mkuu wa timu ya England, Roy Hodgson akiwa hoi.
Mashabiki wa timu ya England wakishangilia baada ya Rooney kufunga bao la kusawazisha dakika ya 75.
ENGLAND imepoteza mechi ya pili mfululizo ya Kundi D Kombe la Dunia, baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Uruguay mjini Sao Paulo, Brazil.
Mbaya wa England alikuwa mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez aliyefunga mabao yote mawili, moja kila kipindi wakati bao pekee la England limefungwa na mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.

Uruguay walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 39, baada ya Luis Suarez kumalizia kazi nzuri ya Cavani.
England walisawazisha dakika ya 75, Wayne Rooney akimalizia vizuri krosi ya Glen Johnsont.

Bao hilo liliwapa tamaa ya mabao zaidi England na kujikuta wanamsahau kidogo Suarez, ambaye alitumia mwanya huo kuwafunga bao la pili dakika ya 85.

Suarez alifunga bao hilo baada ya kuuwahi mpira mrefu wa juu uliomshinda Nahodha wa England, Steven Gerrard na kumtungua Joe Hart.

Kikosi cha Uruguay kilikuwa: Muslera, Gimenez, Godin, Caceres, Pereira/Fucile dk79, Lodeiro/Stuani dk67, Gonzalez, Arevalo Rios, Rodriguez, Cavani na Suarez/Coates dk89.

England: Hart, Baines, Cahill, Jagielka, Johnson, Gerrard, Henderson, Sterling/Barkley dk64, Rooney, Welbeck/Lallana dk71 na Sturridge.
Man of the match: Luis Suarez.

Referee: Carlos Velasco Carballo (Spain).

Attendance: 62,575

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

LAANA

 
Top