0
1403298150791_lc_galleryImage_epa04269872_French_player             
Wachezaji wa Ufaransa wakipongezana baada ya kufuzu hatua ya 16
TIMU ya Taifa ya Ufaransa imeitandika Uswisi mabao 5-2 usiku huu na kufuzu hatua ya 16 ya michauno ya kombe la dunia kutoka kundi E.
Karim Benzema amefunga goli kali dakika ya mwisho, lakini kwa bahati mbaya mwamuzi alikuwa ameshapuliza kipyenga kumaliza mchezo huo.
 
Mabao ya Ufaransa yamefungwa na  Giroud dakika ya 17, Matuidi 18, Valbuena 40, Benzema 67, Sissoko 72.
 
Mabao ya Uswisi yamefungwa na Dzemaili katika dakika ya 81 na Xhaka dakika ya 87.
Katika mchezo wa kwanza wa kundi E, Uswisi walishinda mabao 2-1 dhidi ya Ecuador, wakati Ufaransa waliitandika Honduras mabao 3-0.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

LAANA

 
Top