Lakini pamoja na ukali wa wimbo huu, uliwachukua muda wa nusu saa wakali hawa kukamilisha session ya vocal ndani ya studio za One Love FX, jijini Mwanza chini ya mtayarishaji Tidd Hotter.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Tidd Hotter ameeleza kuwa collabo hiyo ya kwanza kati ya wakali hao ilifanyika kama sehemu ya kipindi cha kituo kimoja cha runinga kilichoko jijini Mwanza, ambacho kina lengo la kuonesha utengenezaji wa nyimbo studio mwanzo hadi mwisho.

“Yaani kile kipindi kinashuti producer anavyoanza kumsikiliza msanii, kazi inavyotengenezwa hadi inavyokuja kuisha inakuaje. Ni kipindi kama cha nusu saa hivi kwa hiyo kazi ilifanyika kama nusu saa pia.” Ameongeza.
Usikose kusikiliza The Jump Off ya 100.5 Times Fm, leo kuanzia saa mbili kamili usiku hadi saa nne usiku utamsikia Tidd Hotter akifunguka zaidi kuhusu kazi zake.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.